Rais wa Marekani Barack Obama anasema utawala wake hauingizi siasa kwenye mashambulizi yaliomuuwa Osama Bin Laden , na kupinga ukosoaji kwamba White house inajitumbukiza katika kusheherekea kupita kiasi juu ya kifo cha kiongozi huyo wa ugaidi.
Akizungumza siku kadhaa kabla ya maadhimisho ya mwaka wa kwanza tangu  mashambulizi ya makomandoo yaliomuuwa kiongozi wa Alqaeda Osama Bin Laden, Bw.Obama alisema jumatatu kuwa kuna wengine  ikiwa ni anaonyesha wazi kumlenga mpinzani wake katika uchaguzi wa Novemba ambao wamebadili misimamo yao juu ya kufanya jambo kama hilo.
Bila kumtaja Romney kwa jina Bw.Obama  alipendekeza kuangalia maelezo ya siku za nyuma ya watu juu ya suala hilo. Romney alisema miaka kadhaa iliyopita kuwa haikuwa na maana yeyote kutumia fedha nyingi kumfuatilia mtu mmoja, lakini Jumatatu alisema kuwa angeagiza Bin Laden auwawe.