Mzee Majuto( Kushoto) akiwa na Sharo milionea
Nguli  wa  sanaa  ya  vichekesho  Bongo,  Amri  Majuto ‘Mzee Majuto’  amesema  anakaribia kuachana na fani hiyo  iliyomletea  umaarufu na heshima kubwa kote nchini.
 Katika mahojiano ya  dakika  20 aliyofanya  na mtandao huu  akiwa  wilayani Bagamoyo Mzee Majuto  alisema kuwa  anataka kufanya kazi zake mwenyewe  sambamba na   vijana wachache aliowachagua   kuepuka  dhuluma anayokutana nayo kutoka kwa wajanja  wanaotajirika kupitia  migogo yao huku  wakitoa  malipo kiduchu kwa wasanii.
“Binafsi nalipwa  Laki tano  mpaka sita  kwa  filamu moja  ambayo  nina uhakika  mtengezaji anakwenda kuingiza  zaidi ya milioni themanini,  sasa  kuna haja gani mimi kuendelea  kufanya kazi  hizo”, alihoji Mzee Majuto.
Akiendela zaidi  mchekeshaji huyo  mwenye heshima kipee kwa wapenzi wa  filamu nchini alisem akuwa  si kama  anaacha  kuigiza moja kwa  moja  lakini atahamia  katika kufanya kazi zake binafi tofauti na hizi za  watu ili aweze kunufaika na jasho lake .
Hivi ninavokwambia tayari nimeshanunua baadhi ya vifaa vya kazi  na baadhi nategemea kuvipata ifikapo mwezi wa 9 mwaka huu ,  alisema   Majuto na kuongeza kuwa  hakika  nitageukia kwenye kufanya kazi zangu mwenyewe  ili na mimi  nifaidi jasho langu”  alimaliza  mchekeshaji huyo
Axact

Axact

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

Post A Comment:

0 comments: