Loading...

OMG!! THIS IS ANOTHER NEW COMPLICATION - SNAKE VS SNAKE. FIGHT TO DEATH ( VIDEO IN SIDE)

Video 61

CHADEMA Yatangaza Kutoshiriki Kura ya Maoni ya Katiba Mpya


DK. Vincent Mashinji Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (chadema), amesema kuwa Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi ndiyo msingi imara pekee unaoweza kuweka mifumo na taasisi kwa ajili ya maendeleo ya kweli yatakayogusa maslahi ya Watanzania wote badala ya nchi kuongozwa na kauli za viongozi.

Kutokana na umuhimu huo wa kuzingatia maoni ya wananchi yanayobeba matakwa yao katika mchakato wa Katiba Mpya, amesema kuwa Chadema hakitashiriki kura ya maoni ya Katiba Mpya Inayopendekezwa ambayo ilipitishwa na Bunge Maalum la Katiba baada ya kubadili na kuondoa mapendekezo yaliyotolewa na wananchi kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya.

Badala yake, Chadema kitaendelea kuweka agenda ya kupigania Katiba Mpya na bora katika vipaumbele vyake, kwa sababu itatibu vidonda na kumaliza makovu yaliyoko katika jamii kutokana na matatizo mbalimbali kama vile ukosefu wa haki, migogoro ya ardhi, wananchi kukosa huduma za msingi za kijamii zikiwemo elimu, maji na afya.

Dkt. Mashinji aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipoukaribisha ujumbe wa Chama cha Centre Party cha Norway uliofika ofisini kwake jijini Dar es Salaam kutia saini makubaliano ya ushirikiano kati ya vyama hivyo kwenye Mradi wa Elimu ya Demokrasia awamu ya pili unaofanyika Wilaya ya Mtwara Vijijini.

Dkt. Mashinji pia amekishukuru chama hicho kwa kusaidia kutoa elimu ya uraia kwa Watanzania hususani maeneo ya vijijini katika mradi ambao unahusisha vyama vyote vya siasa vyenye uwakilishi ndani ya Bunge, huku akisisitiza kuwa Chadema kiko tayari kwa ushirikiano unaozingatia maslahi na matakwa ya wananchi hasa katika kukuza uelewa wa kudai haki, demokrasia na uongozi bora ndani ya nchi.

“Suala la Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi kama ilivyowasilishwa kwenye rasimu ya pili na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya ni agenda muhimu kwa Watanzania wapenda nchi yao na sisi ni kipaumbele kwa mwaka huu na kuendelea hadi hapo nchi yetu itakapopata Katiba Mpya ya Wananchi.

“Jana na leo tumewasikia baadhi ya viongozi wa serikali wakisema kuwa wanajiandaa kuitisha kura ya maoni…hatutashiriki kura ya maoni ya Katiba Mpya Inayopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba. Tunajua Watanzania wengi wanataka Katiba Mpya iliyotokana na maoni yao, si ile iliyochakachuliwa bungeni.

“Katiba Mpya iliweka masuala kuhusu haki za wananchi, kuimarisha misingi na kuweka mifumo ya demokrasia na uongozi bora, walau kwa kuanzia. Hatuwezi kusema sasa tutatumia mikakati gani kuwahamasisha Watanzania kuidai Katiba Mpya…tutajua namna ya kuvuka tukishafika mtoni,” Alisema

Aidha, Katibu Mkuu Dkt. Mashinji alisisitiza kuwa suala la nchi kuwa na misingi na mifumo imara ya demokrasia na uongozi bora ni muhimu kwa Tanzania, katika wakati ambapo nchi inaelekea kwenye uchumi mkubwa wa nishati ya gesi na mafuta, akisema vinginevyo ni hatari iwapo taifa lenye utajiri mkubwa wa rasilimali, litaendelea kuwa na wananchi waliokata tamaa kutokana na mfumo mbovu uliopo.

Kwa upande wake ujumbe huo uliokuwa ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Centre Party, Knut Olsen, ulisema kuwa chama hicho kinashukuru kwa mradi huo kuingia katika hatua ya pili kuanzia mwaka 2016-2019 huku hatua ya kwanza ikiwa na mafanikio makubwa katika jamii ya wananchi wa maeneo ya pembezoni.

“Kama unavyojua, mradi huu kupitia TCD unahusisha vyama vyote vyenye uwakilishi ndani ya bunge, na lengo letu ni kuwajengea uwezo viongozi wa vyama hasa wanawake na vijana katika ngazi ya jamii kwenye vitongoji, vijiji, kata na bunge ili waweze kushiriki mchakato wa maamuzi. Tunatarajia kuendelea kupata ushirikiano katika hatua ya pili,” alisema Inger Bigum, ambaye ni Meneja wa Mradi hapa nchini.

Wengine waliokuwa katika ujumbe huo wa Centre Party ni pamoja na Vijana Sara Hamre Katibu Mkuu wa, Katibu Mkuu wa Wanawake, Eline Stokstad-Oslan na Kristin Madsen Katibu Mkuu wa Wazee.
Mradi huo wa Elimu ya Demokrasia katika Wilaya ya Mtwara Vijijini unaohusisha vyama vyenye uwakilishi bungeni kupitia Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) chini ya ufadhili wa chama hicho, katika awamu ya kwanza ulihusisha kata za Msangamkuu, Nanyamba, Ziwani na Mbembaleo na katika sasa awamu ya pili utakuwa katika kata za Mkunwa, Tangazo, Mayanga na Madimbwa

Magazeti ya Leo Ijumaa ya Tar:- 29.04.2016

Picha 6 za Muonekano wa Daraja la Kisasa la Kigamboni Litakalozinduliwa Leo na Rais Magufuli

Daraja la kisasa la Kigamboni linalounganisha eneo la Kigambonina upande wa Kurasini likikatisha bahari ya Hindi. Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kulizindua rasmi daraja hilo  leo Jumanne Aprili 19, 2016.
Akina mama na watoto wao wakilishangaa daraja hilo la kisasa
Barabara inayoelekea kwenye daraja hilo

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Asema Serikali Itaendelea Kuwatumbua Majipu Wala Rushwa Bila Kujali Hadhi Zao


Serikali  ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli, itaendelea kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi kwa nguvu zote bila kutetereka.

Lengo la hatua hiyo ni kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali na kuboresha uwajibikaji na maadili katika usimamizi wa rasilimali za umma na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alisema hayo katika hotuba yake kwa Taifa wakati wa sherehe ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Hivyo aliwaomba Watanzania wote kuunga mkono kwa vitendo juhudi na maelekezo ya Dk Magufuli za hatua anazozichukua dhidi ya vitendo vya rushwa na ufisadi nchini. 
Kutokana na hatua hizo, Makamu wa Rais alisema hadi sasa jumla ya kesi 596 za rushwa zinaendelea mahakamani na jumla ya Sh 6,543,342,793 tayari zimeokolewa.

“Naomba nitumie fursa hii kuwakumbusha Watanzania wenzangu kujiepusha na vitendo vya kutoa na kupokea rushwa,” alisema Samia na aliwataka watumishi wa umma, watumishi katika sekta binafsi, wajasiriamali na kila mmoja kujiepusha na vitendo vya rushwa na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia katiba, sheria, kanuni, miongozo na taratibu zilizowekwa.

“Kama nilivyokwishasema mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu zinaendelea kuhimiza mapambano dhidi ya Rushwa chini ya kaulimbiu “Timiza Wajibu wako, kata Mnyororo wa Rushwa,” aliongeza Makamu wa Rais.

Samia alisema suala la rushwa limeongelewa mara nyingi na athari zake zinajulikana ikiwa ni pamoja na ubadhirifu wa mali za umma, mikataba isiyofaa kwa taifa na udanganyifu na kupokea fedha ili kukiuka sheria kwa manufaa binafsi huchangia kwa kiwango kikibwa kuwanyima wananchi hazi zao na kudhoofisha ustawi wa taifa letu.

Mbali na hatua hiyo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuendelea na mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, pia alisisitiza kwa mara nyingine kwa kusema kuwa Serikali haina nia ya kumwonea mtu inapochukua hatua ya kutumbua majipu kwa watumishi wa umma.

Akishangiliwa na wananchi wakati akiwahutubia kwenye sherehe hizo, Makamu wa Rais alisema lengo la Serikali la kutumbua majipu ni kurekebisha na kurejesha nidhamu, uadilifu na uwajibikaji serikalini kama ilivyoagizwa katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili Watanzania wote wafaidike na matunda ya nchi yao.

“Mnasikia katika Serikali ya Awamu ya Tano tunarekebishana, majipu yanatumbuliwa ...kwa kweli hatuna nia ya kumwonea mtu, tunarekebishana na hilo ndilo lililomo katika agizo ya Ilani yetu ya CCM ili kuwanufaisha Watanzania wote wafaidi matunda katika nchi yao,” alisema Makamu wa Rais

Sera Ya Rais Magufuli ya Kubana Matumizi Yawaliza Wafanyabiashara Dodoma


Sera ya Rais John Magufuli ya kubana matumizi serikalini imekuwa majanga kwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Dodoma, huku wizara nazo zikionja cha moto. 
Katika kipindi hiki cha kuanza kwa mkutano wa Bunge la Bajeti, wafanyabiashara mkoani hapa wamelalamikia biashara kudorora tofauti na kipindi kilichopita. 
Biashara kubwa zinazofanywa wakati wa vikao vya Bunge ni vyumba vya kulala wageni, usafiri wa teksi, kumbi za mikutano na vyakula. 
Mkutano wa bajeti uliopita, vyumba vya kulala wageni katika mji wa Dodoma vilikuwa vimejaa hata kabla ya kuanza mkutano wa Bunge, lakini hali hiyo imekuwa tofauti baada ya jana karibu nyumba zote za kulala wageni kuwa na nafasi nyingi huku nyingine zikiwa hazina wageni kabisa.
Mkutano huo unaoanza leo kupitisha bajeti za wizara na Serikali Kuu, huwa na mjadala mkali na maofisa wa wizara kutoka vitengo mbalimbali husafiri kutoka Dar es Salaam na sehemu nyingine nchini kwa ajili ya kusaidia utoaji wa majibu na hoja zinazotoka kwa wabunge. 
Kutokana na hali hiyo hoteli, nyumba za kulala wageni hutegemewa kuwa zimeshachukuliwa hadi siku chache kabla ya kuanza kwa mkutano rasmi na mji wa Dodoma huanza kushamiri kibiashara, lakini kutokana na sera ya ubanaji matumizi wa Serikali ya Dk Magufuli, mji huo umepooza kama hauna wageni. 
Hata baadhi ya mawaziri wameeleza kuwa hawatachukua maofisa wengi kutoka wizara wanazozisimamia kwa ajili ya kushughulikia makadirio ya matumizi ya wizara zao, watakapowasilisha ndani ya Bunge, kama ilivyokuwa katika Serikali zilizopita. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, January Makamba alisema wizara yake imepunguza kwa zaidi ya nusu ya maofisa wanaokwenda kuhudhuria vikao hivyo Dodoma. 
“Katika Bunge hili si zaidi ya maofisa 10 watakaohudhuria ambao ni waziri, katibu mkuu na naibu wake, wakurugenzi mazingira, muungano sera na mipango, mhasibu mkuu pamoja na mkurugenzi wa Baraza la Mazingira Tanzania (NEMC),” alisema. 
       

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alisema ingawa wizara yake haijafika muda wa kupanga juu ya maofisa wangapi wanaostahili kuhudhuria vikao hivyo, lakini ni lazima wahakikishe wanapunguza idadi hiyo. 
“Lazima tuangalie umuhimu wa mtu kulingana na sekta yetu ya elimu hatutaweza kuja na watu kama ilivyozoeleka huko nyuma,” alisisitiza Profesa Ndalichako ambaye awali alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini (Necta). 
Katika kuonyesha hatua za ubanaji matumizi zimeanza kuuma katika mji wa Dodoma, mmoja wa wahudumu katika nyumba ya kulala wageni iliyopo eneo la Majengo Mapya ambaye hakutaka jina lake kutajwa alisema: “Mwaka huu hakuna biashara kabisa, hata waliopata watu ni wale ambao wamekuja kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za Mei Mosi zinazofanyika kitaifa hapa Dodoma.” 
Alisema wageni wa vikao vya Bunge la Bajeti huomba nafasi siku tatu kabla ya kuanza kwa vikao, lakini mwaka huu hadi kufikia jana mchana hakuna watu walioonyesha kutaka nafasi katika nyumba hiyo. 
Wafanyabiashara wa saluni ambao nao wanategemea vikao vya Bunge kuongeza mapato yao, walisema hali ya kibiashara ni mbaya na kwamba ina tofauti kubwa na vikao vingine vilivyopita.
Hata bei ya vyakula katika masoko mbalimbali haijapanda kama ilivyokuwa wakati wa vikao vilivyopita, hali iliyokuwa inayowalazimu wakazi wa mji huo kufanya manunuzi wiki moja kabla ya vikao vya Bunge kuanza.
Pia, kwa upande wa wingi wa watu na magari kwenye mji huo hali imekuwa tofauti na vikao vilivyopita vya bajeti, ambavyo kulikuwa na idadi kubwa ya watu siku mbili kabla ya kuanza vikao. 
Kama ilivyo kawaida ya maandalizi ya Bunge, barabara za maeneo mbalimbali mjini hapa zimeanza kufanyiwa ukarabati kwa kuwekewa viraka kwenye maeneo yenye mashimo na usafi kwa kuondoa mchanga barabarani.
Older Posts
© Copyright Hisia za Mwananchi | Designed By 0762388056
Back To Top